20 Januari 2013 - 20:30

Rais wa jamhuri ya Gambia amekubali muswada kuwa siku tatu katika wiki hakutakuwa na kazi kwalengo la wananchi wapate muda wa kufanya ibada na kuendeleza harakati za kilimo

Shirika la habari la Ahlul Bayt(a.s)-ABNA: Yahya Jamih Rais wa jamhuri ya Gambia amepitisha kanuni ya siku nne za kazi na tatu kupumzika kwa wafanya kazi nchini humo pia siku ya ijumaa imeongezwa katika masiku yasikuwa na kazi na kutokana na msemo wake Rais huyo:nikwaajilio watu wapate muda wa kufanya ibada na kuendeleza harakati za kilimo.Kananuni hiyo itaanza kutumika kuanzia mwezi wa pili mwaka huu, naye amesema kuwa kupitishwa kwa kanuni hiyo nikwamujibu wa kutekeleza matakwa ya wananchi wa nchi hiyo. kwakutumika kanuni hiyo siku ya kazi katika nchi hiyo itakuwa ni jumatatu na kuisha siku ya Alhamisi ama kuhusu masaa ya kazi itaanza saa 8 asubuhi na kuisha saa 6 jioni.Katika ujumbe wake kwa wananchi amesema kuwa kwakutumika kwa kanuni hiyo wananchi watapata muda wakutosha wa kufanya ibada na kutekeleza masuala ya kijamii na kilimo katika jamii hiyo.